KUSOMA KITABU CHA ZABURI {DAY 05}

| Makala

KUSOMA KITABU CHA ZABURI 

        DAY 05

Zaburi 21

1  Ee Bwana, mfalme atazifurahia nguvu zako, Na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana.

2  Umempa haja ya moyo wake, Wala hukumzuilia matakwa ya midomo yake.

3  Maana umemsogezea baraka za heri, Umemvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.

4  Alikuomba uhai, ukampa, Muda mrefu wa siku nyingi, milele na milele.

5  Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako, Heshima na adhama waweka juu yake.

6  Maana umemfanya kuwa baraka za milele, Wamfurahisha kwa furaha ya uso wako.

7  Kwa kuwa mfalme humtumaini Bwana, Na kwa fadhili zake Aliye juu hataondoshwa.

8  Mkono wako utawapata adui zako wote, Mkono wako wa kuume utawapata wanaokuchukia.

9  Utawafanya kuwa kama tanuru ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. Bwana atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawala.

10  Matunda yao utayaharibu na kuyaondoa katika nchi, Na wazao wao katika wanadamu.

11  Madhali walinuia kukutenda mabaya, Waliwaza hila wasipate kuitimiza.

12  Kwa maana utawafanya kukupa kisogo, Kwa upote wa uta wako ukiwaelekezea mishale.

13  Ee Bwana, utukuzwe kwa nguvu zako, Nasi tutaimba na kuuhimidi uweza wako.


 

Zaburi 22

1  Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha? Mbona U mbali na wokovu wangu, Na maneno ya kuugua kwangu?

2  Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu Na wakati wa usiku lakini sipati raha.

3  Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli.

4  Baba zetu walikutumaini Wewe, Walitumaini, na Wewe ukawaokoa.

5  Walikulilia Wewe wakaokoka, Walikutumaini wasiaibike.

6  Lakini mimi ni mdudu wala si mtu, Laumu ya wanadamu na mzaha wa watu.

7  Wote wanionao hunicheka sana, Hunifyonya, wakitikisa vichwa vyao;

8  Husema, Umtegemee Bwana; na amponye; Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye.

9  Naam, Wewe ndiwe uliyenitoa tumboni, Ulinitumainisha matitini mwa mama yangu.

10  Kwako nalitupwa tangu tumboni, Toka tumboni mwa mamangu ndiwe Mungu wangu.

11  Usiwe mbali nami maana taabu i karibu, Kwa maana hakuna msaidizi.

12  Mafahali wengi wamenizunguka, Walio hodari wa Bashani wamenisonga;

13  Wananifumbulia vinywa vyao, Kama simba apapuraye na kunguruma.

14  Nimemwagika kama maji, Mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu umekuwa kama nta, Na kuyeyuka ndani ya mtima wangu.

15  Nguvu zangu zimekauka kama gae, Ulimi wangu waambatana na taya zangu; Unaniweka katika mavumbi ya mauti

16  Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenizua mikono na miguu.

17  Naweza kuihesabu mifupa yangu yote; Wao wananitazama na kunikodolea macho.

18  Wanagawanya nguo zangu, Na vazi langu wanalipigia kura.

19  Nawe, Bwana, usiwe mbali, Ee Nguvu zangu, fanya haraka kunisaidia.

20  Uniponye nafsi yangu na upanga, Mpenzi wangu na nguvu za mbwa.

21  Kinywani mwa simba uniokoe; Naam, toka pembe za nyati umenijibu.

22  Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu, Katikati ya kusanyiko nitakusifu.

23  Ninyi mnaomcha Bwana, msifuni, Enyi nyote mlio wazao wa Yakobo, mtukuzeni, Mcheni, enyi nyote mlio wazao wa Israeli.

24  Maana hakulidharau teso la mteswa, Wala hakuchukizwa nalo; Wala hakumficha uso wake, Bali alipomlilia akamsikia.

25  Kwako zinatoka sifa zangu Katika kusanyiko kubwa. Nitaziondoa nadhiri zangu Mbele yao wamchao.

26  Wapole watakula na kushiba, Wamtafutao Bwana watamsifu; Mioyo yenu na iishi milele.

27  Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea Bwana; Jamaa zote za mataifa watamsujudia.

28  Maana ufalme una Bwana, Naye ndiye awatawalaye mataifa.

29  Wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu, Humwinamia wote washukao mavumbini; Naam, yeye asiyeweza kujihuisha nafsi yake,

30  Wazao wake watamtumikia. Zitasimuliwa habari za Bwana, Kwa kizazi kitakachokuja,

31  Nao watawahubiri watakaozaliwa haki yake, Ya kwamba ndiye aliyeyafanya.


 

Zaburi 23

1  Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.

2  Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.

3  Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.

4  Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

5  Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.

6  Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.



 

Zaburi 24

1  Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake.

2  Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha.

3  Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?

4  Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila.

5  Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.

6  Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.

7  Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.

8  Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita.

9  Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.

10  Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Bwana wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.



 

Zaburi 25

1  Ee Bwana, nakuinulia nafsi yangu,

2  Ee Mungu wangu, Nimekutumaini Wewe, nisiaibike, Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda.

3  Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja; Wataaibika watendao uhaini bila sababu.

4  Ee Bwana, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako,

5  Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa.

6  Ee Bwana, kumbuka rehema zako na fadhili zako, Maana zimekuwako tokea zamani.

7  Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, Wala maasi yangu. Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee Bwana kwa ajili ya wema wako.

8  Bwana yu mwema, mwenye adili, Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia.

9  Wenye upole atawaongoza katika hukumu, Wenye upole atawafundisha njia yake.

10  Njia zote za Bwana ni fadhili na kweli, Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.

11  Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, Unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi.

12  Ni nani amchaye Bwana? Atamfundisha katika njia anayoichagua.

13  Nafsi yake itakaa hali ya kufanikiwa; Wazao wake watairithi nchi.

14  Siri ya Bwana iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake.

15  Macho yangu humwelekea Bwana daima, Naye atanitoa miguu yangu katika wavu.

16  Uniangalie na kunifadhili, Maana mimi ni mkiwa na mteswa.

17  Katika shida za moyo wangu unifanyie nafasi, Na kunitoa katika dhiki zangu.

18  Utazame teso langu na taabu yangu; Unisamehe dhambi zangu zote.

19  Uwatazame adui zangu, maana ni wengi, Wananichukia kwa machukio ya ukali.

20  Unilinde nafsi yangu na kuniponya, Nisiaibike, maana nakukimbilia Wewe.

21  Ukamilifu na unyofu zinihifadhi, Maana nakungoja Wewe.

22  Ee Mungu, umkomboe Israeli, Katika taabu zake zote.


 


 SADAKA